
Tetesi za soka Ulaya
Klabu ya Tottenham wamekataa pauni milioni 100 mbele kwa mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane ikiwa watafikiria kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 msimu wa joto wakati atakuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.
Manchester City wanazidi kujiamini kuwa wanaweza kumpata Muingereza Jude Bellingham, 19, msimu wa joto, lakini Real Madrid wanasalia kwenye mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Dortmund.
Mtu mwenye nia ya kuinunua Manchester United Sir Jim Ratcliffe anasema hataki kulipa "bei ya kijinga" kwa klabu hiyo.
Tottenham Hotspur wanatarajiwa kukubaliana na kuondoka kwa meneja wao Muitaliano Antonio Conte, 53, wiki hii, huku mchezaji wa zamani na kocha wa kikosi cha kwanza Mwingereza Ryan Mason, 31, akitarajiwa kuchukua usukani hadi mwisho wa msimu.
Arsenal wako tayari kumpa mchezaji wa Norway Martin Odegaard, 24, mkataba mpya wa kumuweka katika klabu hiyo hadi 2030.
Newcastle United inalenga kumlenga kiungo wa Manchester United Scott McTominay msimu huu wa joto na mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland, 26, anaaminika kuwa tayari kuhama.
Matumaini ya Juventus kumsaini N'Golo Kante, 31, bila malipo msimu wa joto yamekatizwa, huku kiungo huyo wa kati wa Ufaransa akitarajiwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na Chelsea.
Arsenal, Tottenham na West Ham wamemtazama mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Noah Okafor, huku kandarasi ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi ikikamilika msimu wa joto 2024.
Kipa wa Aston Villa aliyeshinda Kombe la Dunia Emiliano Martinez anasisitiza kuwa anapanga kusalia katika klabu hiyo, licha ya kuvutiwa sana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 30.